Monday 31 July 2017

BAGAMOYO MARATHON 2015 Edition


Maudhui yetu mwaka huu ni “ANZA KUKIMBIA, UJIKINGE NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA” yaani “PREVENT NON-COMMUNICABLE DISEASES, START RUNNING”.  Hivyo uzinduzi wa mwaka huu ulifanywa na Mwakilishi wa Waziri wa Afya tarehe 19 Machi 2015 mjini Bagamoyo. Pia uzinduzi ulipata uwakilishi wa Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo na pia Chama cha Riadha Tanzania.



Nia na Madhumuni:
·      KUHAMASISHA AFYA BORA– kutokana na ongezeko kubwa la matukio na vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ambukizwa (Non-Communicable Diseases-NCDs) , Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na wadau mbali mbali inasisitiza mazoezi hasa kutembea, mchaka-mchaka (jogging) na kukimbia kama njia kuu ya kudumisha afya na kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa kama vile kisukari, shinikizo la damu n.k. Mbio hizi zitahamasisha ufanyaji wa mazoezi hasa yale ya kukimbia na hivyo kusaidia kupunguza matukio na vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza.


·      KUKUZA UTALII – kama inavyofahamika Bagamoyo ndiyo mji mkongwe kuliko miji yote nchini Tanzania ambao umepitishwa na UNESCO kuwa eneo la saba lenye uhifadhi wa historia ya kale (Seventh World Heritage Site). Mji huu   ulikuwa moja ya soko kuu la watumwa katika Afrika mashariki na kati, hivyo mbio hizi zitasaidia kuutangaza, kuhamasisha na kukuza utalii katika mji huu muhimu kihistoria nchini na hivyo kuchangia kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya utalii.


·KUCHANGIA MAENDELEO KIUCHUMI – kwa kuwa matarajio yetu ni kuwa na wageni wengi kwa tukio hili katika mji wa Bagamoyo tunatumaini kuwa tukio hili litaongeza shughuli za kibiashara katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo hivyo kuboresha uchumi wa mji huu.


·      KUENDELEZA RIADHA TANZANIA

Na nia ya mwisho, japo ndio kuu hasa, ni kuwajengea uwezo vijana wenye vipaji vya mbio ndefu na baadaye kujenga kambi itakayowawezesha kuwajenga kinidhamu ili waweze kushiriki na kushinda mbio ndefu maarufu duniani siku za usoni. Tunaamini katika maandalizi sahihi ya washiriki ili kurejesha vyema heshima ya Tanzania katika mchezo wa riadha.

Mbio hizi zinatarajia kushirikisha makundi ya mbali mbali ya watu kama ifuatavyo:-
Wakimbiaji wataaluma(professional athletes)
Kilomita 21.1 Umri wa miaka 14 na kuendelea.
Wakimbiaji wengine (casual runners)
KM 10  Umri wa miaka 14 na kuendelea
KM 5    Family Fun Run.
Tamasha hili litajumuisha mbio zifuatazo:-
Mbio ndefu za 21.1 km (Half Marathon) - Mbio hizi zinaratajiwa kuanza saa 12:30 asubuhi (6:30AM sharp) ambapo zitaanzia Uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku kupitia (Mangesani Road) na baadaye, kupitia Bagamoyo Road uelekeo wa Dar es Salaam na kugeuzia maeneo ya Kiromo.
Mbio ndefu za 10.5 km (Quarter Marathon) - Mbio hizi zinaratajiwa kuanza saa 12:45 asubuhi (6:45AM) ambapo zitaanzia Uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku kupitia Mangesani Road, katikati ya mji na kisha kuchukua Bagamoyo Road uelekeo wa Dar es Salaam mpaka makutano ya Barabara ya Msata. Kisha watachukua uelekeo wa kuelekea Msata takribani kilomita nne (4)  ambapo watageuza kurejea uwanja wa shule ya Mbaruku.
Mbio za kujifurahisha (Fun Run) - Mbio hizi zinatarajiwa kuanza saa 01:00 pale uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku kupitia Mangesani Road na  kuelekea upande wa mahoteli ya kitalii mpaka kufika kituo cha zimamoto  ambapo washiriki watageuza kurudi uwanja wa Mbaruku.




Kutembelea sehemu za Kihistoria.

Hii ni nafasi nzuri sana kwa wale watakaweza kufika Bagamoyo siku moja kabla (Jumamosi ya tarehe 13 Juni) na kutembelea sehemu mbalimbali za kihistoria Bagamoyo, kama, Kaole ruins, Kanisa la Mwanzo Africa Mashariki, nk.
Weekend gateaway
Bagamoyo kuna hotel nzuri sana za ufukweni, hivo tunawahimiza hasa watu wa Dar es salaam kufika na ku ‘refresh’ baada ya shughuli za kila siku kwenye jiji letu hili la Dar es salaam. Tungependa sehemu kubwa ya jiji ihamie Bagamoyo wikiendi ya tarehe 14. Mazungumzo yanaendelea na hotel mbali mbali za Bagamoyo ili kupata malazi kwa bei za punguzo.






BURUDANI
Mbdio hizi zinadhaminiwa na Coca Cola, E- Fm; Tanzania Standard News Papers, Azam Media, Oceanic Bay Hotel & Resort , Inoga Hotel na Watu Binafsi. Tupo mbioni pia kukamilisha udhamini kutoka kwa wadau wengine wa Michezo na Afya. Tunaomba ushirikiano kutoka wadau wa michezo na pia watu wote wenye mapenzi mema na mchezo wa riadha ili kuboresha azma yetu. Maelezo zaidi yanapatika kwenye website yetu www.bagamoyomarathon.co.tz 

ZAWADI
Ndugu Waandishi wa Habari, Tunatarajia kuwa na zawadi nono na kwa washiriki wengi, kama ifuatavyo:-

 21.1 km Half Marathon 

 10.5 km Half Marathon 

 Gents 
Ladies 

 Gents 
Ladies 
Mshindi 1
             500,000
          500,000

         100,000
         100,000
Mshindi 2
             400,000
          400,000

           80,000
           80,000
Mshindi 3
             300,000
          300,000

           50,000
           50,000
Mshindi 4
             200,000
          200,000

           40,000
           40,000
Mshindi 5
             150,000
          150,000

           40,000
           40,000
Mshindi 6
             100,000
          100,000

           40,000
           40,000
Mshindi 7
               80,000
            80,000

           40,000
           40,000
Mshindi 8
               50,000
            50,000

           40,000
           40,000
Mshindi 9
               50,000
            50,000

           40,000
           40,000
Mshindi 10
               50,000
            50,000

           40,000
           40,000

 1,880,000
1,880,000

510,000
510,000

UANDIKISHWAJI
Ndugu waandishi wa Habari ,
Uandikishwaji utaanza rasmi siku ya Jumatano tarehe 03 Juni  2014, katika maeneo  yafuatayo:-
·      Tunatarajia kuwa na Vituo mbalimbali jijini na kwa kuanzia tutakuwa Quality Centre na Msasani Mall kwa kuanzia. Vituo vingine tutaendelea kufahamishana kadiri tunavyovipata.


-->

No comments: